arrow-up

Tunapojaribu kutafuta chimbuko la mchezo wa roulette, tunakumbana na sintofahamu nyingi sana. Ijapokuwa hakuna mwenye ushahidi wa hakika, inaaminika pakubwa kuwa mchezo huu ulivumbuliwa kibahati tu, na gwiji mmoja wa hisabati kwa jina Blaise Pascal. Mchezo huu ukianzia karne ya 17 wakati gwiji huyo alipokuwa katika harakati za kuvumbua mashine ya mwendo, kwa kweli mchezo wa Roulette umetoka mbali sana. Baadhi ya ushahidi wa hilo umepatikana na unaashiria ya kwamba vizazi vingi vimekuwa vikicheza mchezo huo ama mifano yake kwa miaka nyingi. Hizi ni baadhi ya mifano kutoka kwa historia za dunia ambazo zinaonyesha dalili ya mchezo wa Roulette ama mifano yake.

Mchezo wa roulette kuzunguka ulaya

Acha tu tuseme kwamba michezo inayochezwa mitandaoni na pia ile inayochezwa mezani katika kasino, haingekua ilivyo sasa iwapo haingepata mchango mkubwa kutoka kwa Louis na Francois Blank. Wawili hawa waliondoa kile kinachojulikana kimombo kama`double zero pocket`, hivyo kutoa nafasi kwa mchezo unaojulikana leo kama Roulette ya ulaya. Hii ilitokea mwaka wa 1842 wakati kamari ilikuwa bado haijahalalishwa nchini ufaransa. Ili kueneza na kukuza mchezo huu, wawili hao iliwabidi waende katika jiji la Hamburg nchini Ujerumani. Walikutana na jamii ya wacheza kamari na kutambulisha kwa wakereketwa aina hiyo mpya ya kucheza mchezo huo. Badala ya kuukataa mfumo huo mpya, jamii hiyo iliupenda na kuunga mkono sana na baada ya kipindi kifupi, mfumo huu mpya wa kucheza Roulette ulikua unatumika karibia kila pembe. Sababu iliyofanya mfumo wa`single zero slot` kupendwa na wengi ilikuwa ile asilimia kubwa ya faida kwa mchezaji ikilinganishwa na faida kwa wamiliki wa kasino. Katika mfumo wa `double zero slot`, wenye kasino walikua na faida ya asilimia 5.26 ikilinganishwa na mfumo mpya wa `single zero slot` ambapo asilimia hiyo ilishuka hadi asilimia 2.70. Kila mtu alikaribisha ongezeko hilo la faida kwa mchezaji katika mfumo mpya. Haikuchukua muda mrefu kwa mfumo wa `double zero slot` kupotea.

Cheza roulette mtandaoni!

Mara nyingi ulisemekana kuwa rahisi zaidi, unaweza kuwa wa kusisimua zaidi ndani ya kasino. Ukitegemea bahati, kucheza mchezo wa roulette hakuhitaji ujuzi wowote maalum ama maktaba iliyojaa vitabu vya hisabati ili kuweza kuucheza.

Acha tujaribu kuelewa vigezo muhimu vya mchezo huu. Mchezo huu una gurudumu lililoandikwa nambari kutoka 1 hadi 36. Gurudumu la roulette linaweza kuwa na sufuri ama, sufuri mara mbili (mfumo wa Marekani). Kuna kipira kidogo na meza ambapo wachezaji hutoa makadirio ya hatma ya mzunguko wa gurudumu.

Mchezo huanza wachezaji wanapokubaliana kiasi cha pesa watakachotoa iwapo matokeo fulani ya mchezo yatapatikana. Kiasi cha pesa hizo hakiruhusiwi kuvuka peo za kiasi cha pesa iliyowekewa meza fulani. Pindi kiasi cha pesa kinapokubaliwa, gurudumu la roulette huzungushwa. Wakati gurudumu linapokuwa likizunguka, kipira kidogo cha roulette hurushwa ndani ya gurudumu hilo linalozunguka. Kipira hicho husimama katika moja ya nambari zilizochorwa katika gurudumu la roulette linapokaribia kuacha kuzunguka. Nambari ambayo kipira hicho kinaishia gurudumu la roulette linapoacha kuzunguka, ndiyo matokeo ya mchezo huo. Washindi hulipwa baada ya pesa za walioshindwa kukusanywa. Mchezo unapoisha meza husafishwa na kutayarishwa tayari kwa mchezo mwengine.

Makadirio ya hatma ya mzunguko wa gurudumu la roulette yanaweza kuwa ya aina tofauti tofauti kulingana na anavyotaka mchezaji. Makadirio yanaweza kugawanywa katika makundi mawili- kadirio za ndani na kadirio za nje. Iwapo kadirio zimewekwa kwa nambari maalum ama seti ya nambari maalum, kadirio hiyo ni ya ndani. Iwapo kadirio imewekwa kwa nambari mbili kwa kuweka vibanzi vya roulette katika mstari unaotenganisha nambari hizo, kadirio hiyo inajulikana kama `straight-up bet`. Pia, unaweza kuweka kadirio ya mgawanyo (split bet) kwa kuweka kadirio kwa nambari tatu zinazofuatana ama kadirio ya ukubwa zaidi ya kona, ya nambari nne zinazofatana. Iwapo mchezaji ataamua kuongeza hadi nambari sita katika kadirio, hata hiyo inaruhusiwa. Kadirio ya ndani ya aina hiyo, inajulikana kama `Six-line bet. ` Katika kasino ambazo kadirio ya aina hii inaruhusiwa, hii huwa kadirio ya juu zaidi ambayo mchezaji wa roulette anaweza kuweka.

Kadirio za nje ndizo ambazo kwa kawaida huwekwa kwa matokeo ya aina nyingi. Matokeo haya yanaweza kuwa rangi, nambari za witiri na sufwa, vigawe vya mbili n.k. ijapokuwa malipo yake yako chini, ni kadirio salama. Hii ndio sababu inayopelekea kila mara wanafunzi wa mchezo wa roulette kushauriwa kuanza na kadirio za nje. Uwezekano wa kupoteza katika kadirio hizi uko chini sana, na hii inatoa nafasi nzuri ya mtu kujifunza zaidi. Nyingi ya kadirio za nje zinalipa 1 kwa 1. Hatahivyo mifumo michache ya kadirio hiyo kama vile kadirio ya safu na kadirio ya dazani hulipa vizuri na kufika hata 2 kwa 1.

Maelekezo kwa wanaoanza kamari

Inawezekana umeshawahi kuiona michezo mingi ya roulette mitandaoni hata kama hujawahi kucheza mchezo huo. Inawezekana umewahi kushawishika kucheza roulette mtandaoni lakini kwa sababu ya kukosa kuujua mchezo huo ukaachana na wazo hilo. Michezo ya mitandaoni ndio tegemeo kubwa la kasino nyingi. Wanapenda sana kuwaacha wachezaji wajaribu ili wajionee. Lazima umeona katika sinema nyingi jinsi mezani panapochezwa mchezo huu panavyokaa. Wakati roulette mtandaoni inaweza kukutia tumbo joto, ni fursa nzuri ya mchezaji kurusha kipira katika nambari za bahati. Nyingi ya kasino sasa zinawapa fursa wachezaji wa kikweli kujaribu roulette za mitandaoni bila malipo. Madhumuni yake ni kuchagua nambari ambayo juu yake kipira kilichorushwa husimama baada ya gurudumu la roulette kuacha kuzunguka. Unaweza kukadiria kwa nambari moja ama uwe salama kwa kufanya kadirio iwe ya zaidi ya tokeo moja.

Kuelewa sheria za gurudumu

Sawa, kuna aina mbili za gurudumu la roulette:

  1. Gurudumu la kiulaya lina nafasi ambazo zina nambari kutoka 0 hadi 36. Kwa hivyo kwa jumla zipo 37. Asilimia ya ushindi kwa wamiliki wa kasino katika gurudumu hili ni 2.63.
  2. Gurudumu la kimarekani pia lina nambari kutoka 0 hadi 36. Lakini zaidi ya hizo, lina nafasi moja zaidi ya 00. Hapa, asilimia ya ushindi ya wamiliki wa kasino ni 5.26.

Haijalishi iwapo mtu atacheza katika kasino ama mtandaoni, vigezo hivi muhimu vya mchezo huu havibadiliki.

Mpangilio

Kwa zilivyopangwa nambari zimewekwa katika orodha. Nje ya eneo hilo kuna vijisanduku vilivyowekwa katika safu tofauti tofauti. Hivyo, utapata nyekundu/nyeusi na pia witiri/sufwa miongoni mwa makundi mengine ya nambari. Nambari zilizopangwa katika mistari 12 ndani ya nambari tatu zinazotengeneza safu 2 za kutoka chini mpaka juu. Nafasi ya sufuri na ile ya sufuri mbili zipo juu kabisa.

Vibanzi na mizozo

Mizozano inaweza kuwa mingi sana katika mchezo wa roulette, hivyo basi ili kuzuia misukumano yoyote, kasino zilivumbua njia nzuri ya kupambana na jambo hilo; kupatiana vibanzi vya rangi tofauti kwa wachezaji tofauti. Njia hii pia inatumika kwa roulette ya bila malipo ya mtandaoni yenye zawadi za fedha. Vibanzi hivyo haviwezi kutumika katika meza zengine, kwa hivyo unahitaji kutoa pesa ili upate vibanzi vipya kila vinapoisha. Kulipia vibanzi kiholela bila kufuata maagizo hakuruhusiwi. Kila meza itakua na kiwango chake cha chini zaidi cha pesa za kuchezea na halkadhalika kiwango cha juu zaidi. Kadirio za ndani na za nje haziwezi kuchanganywa ili kufikia kiwango cha chini zaidi. Idadi ya chini ya dola 5 inamaanisha 5, na haiwezi kugawanywa katikati. Mhudumu atawacha gurudumu la roulette lizunguke kisha ataandika nambari ya mwisho ambayo kipira kitasimamia. Nambari ya ushindi huwa imewekewa alama.

Siri nzuri za kucheza mchezo huu

Iwapo tayari umekadiria nambari yako ya bahati, bado unaweza kukadiria nambari hiyo hiyo tena kwa kuweka vibanzi vyako vya mchezo juu ya vibanzi ulivyoweka mwanzo. Cheza hadi muhudumu aseme `hakuna kucheza zaidi. ` Lakini kumbuka, ijapokuwa inasisimua na kuvutia, wakati wote wamiliki wa kasino huwa katika nafasi bora zaidi. Fata bahati na moyo wako inavyokuambia na bila shaka usisahau kutumia akili na tathmini zako.

Bonasi kwenye 1-th amana 100% hadi $100
Nambari ya bahati
KITOANAMBARI
Siku ya kuzaliwa
Tarehe ya mchezo


 
 
Video za roulette
Jinsi ya Kucheza roulette
Jifunze jinsi ya kucheza roulette ukitumia muelekezo huu. Tutakufundisha jinsi ya kuwa mchezaji wa roulette
Ona video zote
Endelea kuwasiliana nasi
Tafadhali weka anuani yako ya barua pepe hapo chini
na tutakutumia nambari mpya ya bahati kila siku!